IQNA

Serikali ya Nigeria yamuachilia huru Sheikh Zakzaky na mkewe

9:54 - July 29, 2021
Habari ID: 3474137
TEHRAN (IQNA)- Ofisi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria jana usiku iliripoti taarifa ya kutolewa hukumu ya kuachiwa huru Sheikh Zakzaky na mkewe.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Nigeria, Ofisi ya Sheikh Zakzaky imetangaza kuwa mahakama katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria imewafutia tuhuma zote zilizokuwa zikiwakabili Sheikh Zakzaky na mkewe na kuamuru kuachiwa huru. Ofisi hiyo imeongeza kuwa, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe wataachiwa huru karibuni. Hukumu hiyo inatajwa kama ushindi kwa kambi ya muqawama mkabala wa ukandamizaji na dhulma kubwa ya serikali ya Nigeria.  

Serikali ya Nigeria hadi kufikia sasa ilikuwa imezuia kuachiwa huru mwanazuoni huyo mtajika wa Nigeria na mkewe kwa visingizio mbalimbali na hata kuwanyima ruhusa ya kwenda kupatiwa matibabu. 

Katika miezi ya karibuni ambapo hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky ilizidi kudhoofu taasisi mbalimbali za kutetea haki za binadamu zilitoa mwito mara kadhaa zikitaka kuachiwa huru Kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria. 

3987150

captcha