Duru hiyo Iliandaliwa katika Kituo cha Hayat al-Huda jijini Madina Jumatano usiku.
Maqari mashuhuri Mehdi Adeli na Masoud Movahedirad walisoma Qur’ani Tukufu katika hafla hiyo.
Adeli alisoma Aya za 64-69 za Surah An-Nisa na Movahedirad akasoma Aya za 101-108 za Surah Al-Anbiya.
Programu hiyo pia ilijumuisha qasida ya la Kundi la Al-Ibad.
Kila mwaka Waislamu zaidi ya milioni kutoka duniani kote hukusanyika Makka kwa ajili ya Hija katika mwezi wa Dhul Hijja.
Iran pia hutuma mahujaji pamoja na kundi la wasomaji Qur'ani ambalo ni maarufu kama Msafara wa Nur wa Qur’ani Tukufu.
Wajumbe wa msafara huo huwa na vikao vya kusoma Qur'ani nyakati mbali mbali katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.
4219222