IQNA

Wanawake katika Msafara wa Noor wa Iran washiriki katika vikao vya Qur'ani katika Arbaeen

15:03 - August 19, 2024
Habari ID: 3479300
IQNA - Wanachama wa kike wa Msafara wa Qur'ani wa Arbaeen wa Iran, unaojulikana kama Msafara wa Noor, wameanza kuandaa programu za Qur'ani kwa ajili ya mazuwar.

Wanawake wa Kiirani wanaharakati wa Qur'ani, wakiwemo wasomaji wa Qur'ani  na Tawasheeh, wameanza programu zao katika mji mtakatifu wa Najaf.

 Walianza kutekeleza vipindi vya usomaji wa Qur'ani na Tawasheeh (nyimbo za dini) mjini siku ya Jumamosi.

Nasibeh Karami Parsa, Atefeh Naseh na Zahra Sohrabi hadi sasa wameshafanya kisomo cha Qur'ani, usomaji wa Tarteel na usomaji wa Ibtihal katika duru nne za Qur'ani huko Najaf.

Vile vile, kikundi cha waimbaji qaswida cha Afaq kutoka Mkoa wa Tehran kilikuwa na maonyesho katika haram tukufu ya Imam Ali (AS), ambayo yalipokelewa kwa furaha na mazuwar.

Wanawake wa Kiirani wanaharakati wa Qur'ani kisha waliondoka kuelekea Karbala siku ya Jumapili.

Watarejea Iran siku ya Alhamisi na kundi jingine la wanawake wanaharakati wa Qur'ani kisha watasafiri hadi Iraq kwa ajili ya programu za Qur'ani.

Iranian Noor Convoy’s Women Hold Quranic Programs for Arbaeen Pilgrims

Iranian Noor Convoy’s Women Hold Quranic Programs for Arbaeen Pilgrims

Mjumuiko wa maombolezo ya Arbaeen ni mojawapo ya mikusanyiko mikubwa ya kidini duniani.

Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu  wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdi na jeshi katili la la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.

Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi kubwa ya wasiokuwa Mashia humiminika  katika mji Karbala nchini Iraq, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) ili kushiriki katika shughuli za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala. Arbaeen ya mwaka huu inatarajiwa kuanguka mnamo Agosti 25, kulingana na kuonekana kwa mwezi.

Harakati ya mapambano ya Imam Hussein (AS) dhidi ya dhulma na ufisadi wa utawala wa Bani Umayya ilijaa hamasa, kujitolea na kusabilia kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu, na kwa sababu hiyo imegusa sana nyoyo za Waislamu na hata wapenda haki na kweli wasio Waislamu. Harakati hiyo ya Imam Hussein (AS) inaendelea kuibua vuguvugu na hamasa ya aina yake ndani ya nafsi za wapenzi wa mtukufu huyo.

 3489556

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: arbaeen msafara wa nur
captcha