Sheikh Issa Qassim amesema kumshambulia kiongozi huyu wa juu ni kuuvunjia heshima Umma mzima wa Kiislamu na matukufu yake.
Sheikh Issa Qassim ambaye ni mmoja wa Marjaa Taqlidi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wa nchini Bahrain ametoa taarifa akimwelezea Ayatullah Khamenei Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni nembo adhimu ya Qur'ani na kiongozi adimu katika zama hizi. Ameongeza kuwa, Ayatullah Khamenei amekuwa na mchango mkubwa katika kuuelimisha na kuutia nguvu Umma wa Kiislamu.
Kiongozi huyo wa Bahrain ameongeza kuwa: Kumlenga Ayatullah Khamenei na maneno yoyote ya kumvunjia heshima au vitisho ni sawa na kuudhihaki Umma wote wa Kiislamu, matukufu na nafasi tukufu ya faqihi mtawala.
Sheikh Issa Qassem amesema hatua ya Trump ya kumvunjia heshima na kumtishia kiongozi huyu wa juu ni upumbavu unaosababishwa na kutokuwa makini katika kutathmini mambo na taathira zake.
4292351