IQNA

Nabii Ismail (as) ; Mtoto wa Nabii Ibrahim ( as)

Mtazamo wa Kitaalamu: Kuelewa maana ya Kujitolea Kweli Katika Hija

8:18 - June 19, 2024
Habari ID: 3478981
Mtaalamu wa kitaaluma na kidini wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anasema kiini cha ibada ya Hija ni kuacha matamanio ya kibinafsi na kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu.

Akizungumza na IQNA, msomi wa masomo ya dini na mhadhiri wa chuo kikuu Ismail Mansouri Larijani amefafanua juu ya kiini cha ibada ya Hija na kitendo cha kujitoa mhanga, knachofuata ni mukhtasari wa matamshi yake.

Moja ya miujiza ya Nabii Ibrahim (AS) ilikuwa ni tukio la kumchinja mwanawe, Ismail (AS), Nabii Ibrahim (AS0 ana ndoto ya kumtoa mwanawe kafara, kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, alisema; ewe mwanangu! Ninaona katika ndoto kwamba ninakutolea dhabihu, sema fikira yako,mtazamo wako

Akasema, ‘Baba! Fanya chochote ulichoamriwa na Mwenyezi Mungu akipenda utanikuta mimi ni  mvumilivu, Surah Al -Saffat, Aya ya 102.

 Katika mazungumzo hayo, tunashuhudia kiini cha tauhidi cha Nabii Ibrahim (AS) hakuwahi kuhoji ukweli wa ndoto yake, na Nabii Ismail (AS) hakupinga ujumbe wa mwenyezi mungu na wa baba yake, aliukubali kikamilifu badala yake.

 Hivyo basi, kitendo cha kujisalimisha ni sawa na kufanya kitendo chenyewe.

Hii ndiyo sababu, ingawa Nabii Ismail (as) hakutolewa mhanga, alipata jina la “Zabihullah” kwa sababu alikubali kwa hiari ukweli wa dhabihu, na kukubalika huko ni muhimu.

Ufahamu huu unatusaidia kufahamu maana za kina zilizopachikwa katika taratibu za Hija ya Nabii  Ibrahimu (AS).

 Eid Al-Adh’ha; Mazoezi ya Kujitolea kwa Mwenyewe kwa ajili ya Mwenyezi  Mungu.

 Aya inayofuata inaeleza hivi; “Basi waliposalimu amri wote wawili, naye akamlaza juu ya paji la uso wake,” ikionyesha kwamba juu ya kujisalimisha kwao kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu, hata angejitahidi vipi, kisu hakingekata, Nabii  Ibrahim  (AS) alinoa tena ule ubao, lakini ulibaki butu.

Ilikuwa ni wakati huu ambapo wito wa Mwenyezi Mungu ulikuja; Ewe Ibrahim, Hakika umetimiza maono yako!” Ikafahamishwa kwa Nabii Ibraahimu (AS);  kwamba wajibu wao umekamilika na usalimishaji wao umekubaliwa, “Na hivi ndivyo tunavyo walipa watu wema! Hakika huu ulikuwa ni mtihani ulio dhahiri.

 Asili inayowasilishwa na aya hizi ni utiifu; kusalimisha roho ya mtu kwa Mwenyezi Mungu, mtu anapojisalimisha kwa mwenyzi mungu, hashindwi na tamaa za kidunia.

 Kwa hali hiyo, msingi wa dhabihu wakati wa hija ni kwa waumini kutoa sadaka na matakwa yao binafsi katika kuacha matamanio haya, mtu anakuwa kweli Hija mwenye kuhiji.

 Na vile vile Imam Ali (AS) anatufundisha kwamba: "Kila sala ni madhabahu, hii inaashiria kwamba mtu anapoanzisha swala kwa "Takbir Al-Ihram," wanatangaza kwamba wote isipokuwa Mwenyezi Mungu ni haramu kwao, na wanapotangaza "Allahu Akbar," ni kana kwamba wanajitolea kila kitu ambacho hukengeusha kutoka kwa mwenyezi mungu mmoja. 

Hivyo, mtu mcha Mungu lazima aweke kando matamanio yake binafsi kwa kila sala, jambo ambalo husisitizwa kila mwaka wakati wa hija.

Na vile vile Iwapo hujaji atarudi kutoka hija akiwa huru kutokana na athari za matamanio ya kidunia, wanapaswa kushukuru kwa kujitolea kwao kukubaliwa hija zao na vinginevyo, uchinjaji utakuwa ni nembo bila kuwepo faida za kiroho.

 

3488798

captcha