Kwa mujibu wa msemaji wa wizara hiyo, Abbas al-Bahadli, wafanyaziara hao walitoka katika nchi 140 tofauti kushiriki katika tukio hilo tukufu.
Ziara ya Arbaeen, inayofanyika kila mwaka mjini Karbala, huadhimisha siku ya arubaini baada ya Ashura. kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (A.S.) mnamo mwaka 61 Hijria sawa 680 Miladia. Ni miongoni mwa mikusanyiko mikubwa zaidi ya amani duniani, ikiwavutia mamilioni ya waumini kutoka pembe zote za dunia. Wengi husafiri kwa miguu kutoka Najaf hadi Karbala, safari ya takriban kilomita 80 , huku wengine wakifika moja kwa moja kutoka mataifa ya mbali kuungana na waumini wengine katika maadhimisho hayo.
Maafisa wa usalama wameripoti kuwa hakukuwa na tishio lolote wakati wa tukio hilo. Mkuu wa Kitengo cha Habari za Usalama cha Iraq alisema awali kuwa “hakuna hatari za kiusalama zilizorekodiwa hadi sasa” katika kipindi chote cha ziara hiyo.
Gavana wa Karbala aliongeza kuwa idadi ya wageni imeongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita, ambapo zaidi ya wafanyaziara milioni 21, wakiwemo Wairaqi na wageni kutoka mataifa mbalimbali walihudhuria.
Arbaeen inajulikana si kwa thamani yake ya kidini pekee, bali pia kwa dhihirisho la ukarimu na mshikamano. Maelfu ya mawkib, mabanda ya huduma mbali mbali, huandaliwa, yakitoa chakula, maji, na eneo la kupumbzika bila malipo yoyote kwa wageni.Wafanyaziara kutoka mataifa na tamaduni mbalimbali husafiri pamoja, wakishirikiana safari katika mazingira ya umoja na imani.
/3494251