Hujjatul Islam Seyed Mostafa Hosseini, Katibu wa Baraza la Maendeleo ya Utamaduni wa Qur’ani, alitoa kauli hiyo katika mahojiano na IQNA kwenye Mawkib ya Qur’ani ya Arbaeen, iliyo katika njia ya Najaf hadi Karbala nchini Iraq.
Mawkib ni vituo vya huduma vilivyo katika maeneo ya kidini ya Waislamu wa madhehebu ya Shia au wakati wa matukio ya kidini ya Mashia ambapo wafanyaziara na watu wanaweza kupokea chakula, chai, na sharbat (vinywaji vitamu) na kupata sehemu ya kupumzika.
Hujjatul Islam Seyed Mostafa Hosseini amesema kuwa Arbaeen inatufunulia hazina zake zilizofichika katika nyanja za kijamii na za ukakamavu wa kiroho, hususan katika kusambaza elimu ya Qur’ani Tukufu.
Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkoa wa Zanjan ameongeza: “Kwa miaka kadhaa sasa, tumeshuhudia ukuaji wa shughuli za Qur’ani katika njia ya Arbaeen.”
Kila mwaka, idadi kubwa ya shughuli za aina mbalimbali za Qur’ani hufanyika kwa ajili ya wafanyaziyara wa Arbaeen katika njia hii, amesema Hujjatul Islam Hosseini.
Ameeleza kuwa uandamani wa Qur’ani Tukufu na Ahlul-Bayt (A.S.) unazidi kujitokeza kwa uwazi zaidi kila siku wakati wa maandamano ya Arbaeen, akiyataja maandamano haya kama “mkusanyiko wa majeshi ya Imam Zaman (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake kwa faraja).”
Arbaeen ni tukio la kidini linaloenziwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia siku ya arubaini baada ya Ashura, kukumbuka kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (A.S.), mjukuu wa Mtume Muhammad (S.A.W.) na Imamu wa tatu wa Shia.
Ni miongoni mwa hija kubwa zaidi duniani, ikiwakutanisha mamilioni ya Waislamu wa Shia, pamoja na baadhi ya Waislamu wa Sunni na wafuasi wa dini nyingine, wakisafiri kwa miguu kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Siku ya Arbaeen mwaka 2025 iliangukia Alhamisi, Agosti 14.
Mwaka huu, matembezi ya Arbaeen yamekuwa na programu mbalimbali za Qur’ani. Kama ilivyo desturi ya miaka iliyopita, Iran imetuma msafara wa Qur’ani kuelekea Iraq wakati wa ziara hii.
Wanachama wa msafara huu hufanya shughuli mbalimbali za Qur’ani na kidini, ikiwemo qira’a ya Qur’ani Tukufu, Adhana, na Tawasheeh, katika barabara ya Najaf hadi Karbala na maeneo mengine wakati wa matembezi ya Arbaeen.
Msafara wa mwaka huu unafanya kazi chini ya jina la “Msafara wa Imam Ridha (A.S.).”
3494253