Waislamu hao waliotemebea kwa miguu kuelekea Karbala wakitokea pande tofauti wamekusanyika kwenye Haram ya Imam Hussein (AS) kuadhimisha tukio hilo.
Kandokando ya njia za kuelekea Karbala, maelfu ya 'mawaakib', au vituo vya huduma za kujitolea, zinaonekana zikitoa sadaka za chakula bila malipo, pamoja na maji, matibabu, na sehemu za kupumzikia kwa mazuwari wa Matembezi ya Arubaini.
Matembezi ya Arubaini ni moja ya mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini ya kila mwaka duniani, ambapo washiriki wanamuenzi Imamu huyo wa tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, anayetambulika kama nembo kuu ya kupambana na dhulma, ukandamizaji na uonevu.
Imam Hussein (AS) na masahaba zake 72 waliuawa shahidi katika Vita vya Karbala kusini mwa Iraq mwaka 680 Miladia katika mapambano na jeshi kubwa la mtawala jeuri na dhalimu wa wakati huo wa Bani Umayya, Yazid bin Muawiya.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde wafanyaziara 5,291,005 wamevuka vituo sita vya mpaka wa Iran na Iraq katika muda wa wiki tatu zilizopita kwa ajili ya Matembezi ya Arubaini.
Wakati huohuo, mamilioni ya Waislamu katika miji zaidi ya 500 ya nchini Iran wameshiriki kwenye matembezi yaliyofanyika kwa anuani ya "Walioachwa Nyuma Katika Arubaini," iliyoshirikisha wale wote ambao hawakuweza kusafiri hadi Karbala kushiriki katika Arubaini ya Imam Hussein AS.
Katika mji mkuu Tehran, wananchi Waislamu wa Iran wametembea masafa ya kilomita 13 kutoka uwanja wa Imam Hussein hadi kwenye Ziara la Shah Abdol-Azim Hasani katika mji wa Rey ulioko kusini mwa Tehran..
4299862