IQNA

Imamu Hussein (AS) karbala

Mtazamo wa Qur'ani Tukufu kuhusu mwamko wa Imam Hussein (AS) katika Siku ya Ashura

10:39 - July 07, 2024
Habari ID: 3479082
IQNA- Imam Hussein (AS) alidhulumiwa na baadhi ya vipimo vingine vya mwamko wa Ashura vinaweza kuonekana katika baadhi ya aya za Qur’ani Tukufu.

Imam Hussein (AS) alisimama dhidi ya utawala dhalimu na haramu wa Yazid.

Mwanzoni, hakuna mtu aliyemsaidia hata mmoja katika suala hilo, Kisha yeye na masahaba zake walizingirwa na kuuawa kishahidi katika vita vya umwagaji damu huko Karbala. 

 Kutokana na kipengele hiki, ukandamizaji unaweza kuwa mfano wa kile ambacho baadhi ya aya za Qur'ani zinarejelea.

 Katika aya ya Qur’ani Tukufu imesisitizwa kwamba kama mtu atauawa kwa dhulma na isivyo haki, warithi wa mtu huyo wanaweza kudai Qisas (haki ya kulipiza kisasi): “Msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu Ameiharamisha isipokuwa kwa haki. Akiuliwa kwa dhulma, basi tumempa mrithi wake mamlaka.

Lakini asiruke mpaka katika kuua, kwani atasaidiwa, katika Aya ya 33 ya Surah Al-Isra.

 Heshima kwa maisha ya watu inaonekana katika dini na tamaduni zote.

Lakini kuna Hadithi ambazo kwa mujibu wake kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba zake kunatajwa kuwa ni mfano wa wazi wa mauaji ya kidhalimu.

 Pia, kwa mujibu wa Hadithi hizi, mrithi ambaye ana haki ya kudai haki kwa damu ya Imam Hussein (AS) ni Imam Mahdi (AS), mwokozi aliyeahidiwa.

 Katika aya nyingine, Mwenyezi Mungu anasema kwamba mtu aliyedhulumiwa ana haki ya kuingia katika vita ili kujilinda: “Basi, wamepewa ruhusa ya kushika silaha wale wanaoshambuliwa; wamedhulumiwa, Mwenyezi Mungu ana uwezo wote wa kuleta ushindi." Aya ya 39 ya Surah Hija.

Kwa mujibu wa Hadith, Mwenyezi Mungu alimwambia Ibrahim (AS) kuhusu yale yatakayomtokea Imam Hussein (AS) na Ibrahim (AS) alilia sana.

 Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, katika aya hii pia inahusu ukandamizaji wa Imam Hussein (AS).

 Katika kisa cha Nabii  Ibrahim (AS) na Nabii Ismail (AS), tunasoma kwamba Nabii Ibrahim (AS) aliamrishwa kumchinja mwanawe na kisha Mwenyezi Mungu akampelekea kondoo dume ili atolewe kafara badala ya Nabii Ismail(AS)  Katika Qur’ani, badala yake imetajwa kuwa ni dhabihu kubwa; Basi tukamkomboa kwa dhabihu kubwa,"  Aya ya 107 ya Surah As-Saffat.

3489019

captcha