IQNA

Waislamu wa Ireland

Ireland: Waislamu Wazindua Kampeni ya Kuchangisha Fedha kwa ajili ya Msikiti Mpya huko Tullamore

14:50 - July 22, 2024
Habari ID: 3479170
Kundi la jumuiya ya Kiislamu limeanzisha kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya msikiti mpya huko Tullamore, Ireland.

 Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Midlands Tullamore (MICCT) kilianza kampeni kwenye GoFundMe kutokana na jamii kuzidisha eneo walilokodisha la sasa, ambalo linaelezwa kuwa "dogo," Offaly Live iliripoti Jumatatu.

Kwa mujibu wa taarifa kwenye ukurasa wa uchangishaji fedha, idadi ya Waislamu mjini Tullamore sasa imepita 500, na mali iliyokodishwa kwa ajili ya sala ya kila siku na Ijumaa "haitoshi tena kwa mahitaji ya jumuiya."

 MICCT inalenga kununua eneo la kudumu la kukarabati kuwa msikiti na kituo cha Kiislamu ili kurahisisha maombi, huduma za jamii na madarasa ya Kurani kwa watoto wa Kiislamu.

Ireland: Tralee kupata Msikiti Mpya na Kituo cha Jumuiya ifikapo 2025

Ujumbe kuhusu uchangishaji, ambao hadi sasa umechangisha zaidi ya €1,700 kati ya lengo lake la yuro €250,000, unasema, "Kwa sasa tuna  kwa yuro €200,000 kutoka kwa michango ya ndani lakini tunahitaji  yuro €250,000 zaidi ili kununua na kukarabati mali ya ndani.

3489215

Kishikizo: ireland waislam misitiki
captcha