IQNA

Wazayuni wa Israel waendeleza njama za kuuyahudisha Msikiti wa Nabii Ibrahim AS

23:08 - February 17, 2022
Habari ID: 3474940
TEHRAN (IQNA)- Afisa mwandamizi wa Palestina amesema askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameuhujumu tena Msikiti wa Nabii Ibrahim -Amani ya Mwenyezi Mungu iwe Juu Yake- kwa lengo la Kuyahudisha eneo takatifu la Waislamu.

Mkurugenzi wa Wakfu mjini Al Khali, Jamal Abu Aram amesema wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wameweka ngazi mpya ya umeme katika upande wa mashariki msikini hapo ili Wazayuni waweze kutekeleza ibada katika eneo hilo

Amesisitiza kuwa, hatua hizo za Israel katika uwanja wa Msikiti wa Nabii Ibrahim AS, ni kinyume cha sheria zote na zikiwemo za Umoja wa Mataifa.

Msikiti wa Ibrahim AS ambao ni eneo takatifu kwa Waislamu na Mayahudi  ni Haram Takatifu na uko katika kitongoji cha kale cha Al Khalil  kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel. Kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi, ndani ya msikiti huo kuna kaburi la Nabii Ibrahim AS na mkewe Sarah na vile vile makaburi ya Manabii Is-haq na Yaaqub AS na ya wake zao.

Itakumbukuwa kuwa mnamo mwezi Julai mwaka 2017, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilitangaza kuwa mji wa Al Khalil ulioko Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan ambao ni moja ya turathi za kimataifa unakabiliwa na hatari kutokana na sera haribifu za utawala wa Kizayuni.

3477847

captcha