IQNA

Wazayuni waushambulia tena Msikiti wa Nabii Ibrahim AS

10:25 - March 22, 2022
Habari ID: 3475064
TEHRAN (IQNA)- Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamevamia Msikiti wa Nabii Ibrahim AS katika Ukingo wa Magahribi Jumapili na kupanda juu ya paa la msikiti huo.

Mkurugenzi wa msikiti huo Ghassan al Rajabi amesema wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel watekeleza hujuma hiyo huku wakiwazuia Waislamu kusali katika eneo hilo takatifu.

Amelaani vikali hujuma hujuma dhidi ya eneo hilo na kusema nisehemu ya uchokozei wa kila siku dhidi ya msikiti huo ambao hutekelezwa kila siku na wanajeshi wa Israel na walowezi wa Kizyauni.

Msikiti wa Ibrahim AS ambao ni eneo takatifu kwa Waislamu na Mayahudi  ni Haram Takatifu na uko katika kitongoji cha kale cha Al Khalil  kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel. Kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi, ndani ya msikiti huo kuna kaburi la Nabii Ibrahim AS na mkewe Sarah na vile vile makaburi ya Manabii Is-haq na Yaaqub AS na ya wake zao.

Itakumbukuwa kuwa mnamo mwezi Julai mwaka 2017, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilitangaza kuwa mji wa Al Khalil ulioko Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan ambao ni moja ya turathi za kimataifa unakabiliwa na hatari kutokana na sera haribifu za utawala wa Kizayuni.

3478250

 

captcha