IQNA

Arbaeen

Msafara wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa waandaa vikao vya Qur’ani Najaf

23:06 - August 28, 2024
Habari ID: 3479339
IQNA - Ujumbe wa wasomaji Qur’ani wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa  cha Iran ambao umesafiri hadi Iraq kwa ajili ya Arbaeen ulifanya programu kadhaa za usomaji wa Qur'ani katika mji mtakatifu wa Najaf.

Moja ya programu iliandaliwa katika haram tukufu ya Imam Ali (AS) na nyingine katika nyumba ya kihistoria huko Najaf ambako marehemu mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini (RA) aliishi miaka ya 1960 na 1970.

Msafara wa Qur'ani wa chuo hicho unajumuisha wasomaji Qur’ani kutoka nchi tofauti kama India, Afghanistan, Pakistan, Mali, Nigeria, Burkina Faso, Iraq na Tajikistan.

Wakati wa kukaa kwao kwa siku nane nchini Iraq, wanachama wa msafara huo waliandaa programu mbalimbali zikiwemo za usomaji wa Qur'an, usomaji wa Tarteel, Tawasheeh, Adhana na mashairi ya maombolezi.

Kujibu maswali ya Qur'ani ya mahujaji wa Arbaeen pia ilikuwa kwenye ajenda ya kundi hilo.

Walishiriki katika safari hiyo ya kiroho kwa lengo la kutoa huduma za Qur'ani kwa wafanyaziara wa Arbaeen.

3489668

Kishikizo: arbaeen qurani tukufu
captcha