IQNA

Wanamichezo Waislamu

Msenegali anayechezea Bayern anaipenda Qur’ani Tukufu

12:07 - March 21, 2023
Habari ID: 3476736
Tehran (IQNA) - Picha za Sadio Mane mchezaji wa Timu ya Soka ya Taifa ya Senegal ambaye pia ni mchezaji wa Klabu Bayern Munich ya Ujerumani akisoma Qur’ani Tukufu imesambaa katika mitandao kijamii na kuwavutia .

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,Sadio Mane ameonekana akisoma Qur’ani Tukufu ndani ya ndege  kabla ya mechi dhidi ya Bayer Leverkusen na kuvuia hisia chanya miongoni mwa Waislamu kwenye mitandao ya kijamii.

Thomas Müller, mchezaji wa Ujerumani wa Bayern Munich, alichapisha picha yake akiwa na Sadio Mane, mchezaji mwenzake Muislamu   akiwa anasoma Qur'ani Tukufu wakiwa ndani ya ndege.

Sadio Mane ni maarufu sana mingoni mwa Waislamu duniani kwa sababu ya kujitolea kwake katika kufungamana na mafundisho ya Uislamu.

Katika mahojiano na Daily Mail, mchezaji huyu wa Senegal alisisitiza kuwa hajawahi kugusa pombe katika maisha yake yote.

4129069

captcha