Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika mji wa Shiraz kusini mwa Iran siku ya Jumatatu, Hujjatul Islam Seyed Issa Mostarhami, naibu wa kamati ya kisayansi wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, alisema kongamano hilo linaandaliwa na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa kwa lengo la kuhudumia Qur'ani Tukufu. na kubainisha fikra za Qur'ani za Imam Khamenei.
Alisema zaidi ya vituo 180 vimeshirikiana katika kuandaa hafla hiyo ya kielimu.
Vikao vya maandalizi 200 na warsha 73 za kisayansi zimefanyika kuhusu mada ya kongamano hilo, alibainisha.
Hujjatul Islam Mostarhami aliongeza kuwa makala 2,977 za mukhtasari na makala 2,156 kamili katika lugha 22 za wasomi kutoka nchi 30 zimewasilishwa kwa sekretarieti ya kongamano.
Kati ya makala hizo zote, 845 zimekubaliwa, nusu yake zimechapishwa na zingine zitapatikana katika muundo wa dijiti, alisema.
Pia akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari alikuwa ni Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Shah Cheragh (AS) Hujjatul Islam Ebrahim Kalantari.
Alisema eneo hilo takatifu jijini Shiraz litaandaa kongamano hilo Jumatano, Novemba 13, 2024.
Ameashiria vipengele vitatu muhimu vya kongamano hilo, akisema la kwanza ni kusisitiza umuhimu wa Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu na kwa wanadamu.
Ameongeza kuwa, kipengele cha pili ni kutilia mkazo katika kutambulisha fikra za Qur'ani za Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Suala la tatu ni kutilia mkazo ukweli kwamba Iran ya Kiislamu inaongozwa kwa kuzingatia mafundisho na fikra za Qur'ani.
Masuala ya hivi sasa ya ulimwengu wa Kiislamu, ikiwa ni pamoja na hali ya Ukanda wa Gaza na Lebanon na mapambano dhidi ya ubeberu wa kimataifa pia yatajadiliwa katika kongamano hilo, aliendelea kusema.
3490651