Tukio hilo lilitokea Jumamosi wakati Corbyn, kiongozi mashuhuri wa zamani wa Chama cha Leba, alipokuwa akikaribia kuingia ndani ya jengo hilo, kwani alikuwa miongoni mwa wazungumzaji katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafuasi wa genge hilo la Wazayuni walimwendea, wakimpigia kelele na kumshutumu kwa chuki kabla ya hotuba yake katika kikao kuhusu ubaguzi wa rangi na chuki.
Maafisa wa usalama walingilia kati kuzuia ghasia zaidi.
Baadaye, vizuizi viliwekwa kati ya ukumbi na magenge ya waungako mkono Israel, ambao walikuwa wameshikilia bango lililodai: “Acheni uwongo. Hakuna mauaji ya kimbari huko Gaza."
Katika hujuma inayoendelea ya miezi 13 katika Ukanda wa Gaza, jeshi katili la utawala haramu wa Israel limeua zaidi ya watu 44,000 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 103,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, huku wakiacha eneo hilo haliwezi kukaliwa na watu na kukata sehemu kubwa ya chakula, maji. , dawa, na misaada ya kibinadamu. Israel pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kwa hatua zake huko Gaza.
Corbyn alihutubia waliohudhuria katika jopo lililoitwa: "Baada ya Trump kushinda: Kupinga kuimarika kwa mrengo wa kulia wa kimataifa - Kupinga ubaguzi wa rangi, chuki dhidi Uislamu na chuki dhidi ya Wayahudi."
3490715