IQNA

Jinai za Israel

Hizbullah yampongeza Shahidi Afif kama mpiganaji mara kwenye njia ya muqawama

14:23 - November 18, 2024
Habari ID: 3479769
IQNA - Harakati ya Muqawama ya Lebanon, Hizbullah,  imetoa rambirambi kwa kuuawa shahidi Mohammad Afif al-Nablusi katika shambulio la Israel lililolenga jengo moja katikati mwa Beirut.

Afif alikuwa msemaji wa Hizbullah.

Hizullah ilisema katika taarifa yake kwamba alikuwa mwanamapambano mashuhuri ambaye alikuwa na msimamo thabiti kwenye njia ya Muqawama.

Aliuawa kishahidi baada ya miaka mingi ya kujitahidi kwa utukufu katika nyanja za vyombo vya habari kwenye njia ya Muqawama,  Hizbullah imesema.

Taarifa hiyo imesisitiza kuendelea kwa njia ya mashahidi na kuapa kwamba kumbukumbu zao hazitasahaulika.

Hizbullah pia iliapa kwamba utawala wa Kizayuni utalipa pakubwa kwa jinai zake.

Brigedi za Ezzudin Al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imetuma rambirambi juu ya kuuawa shahidi Afif, na kubainisha kuwa alikuwa na jukumu kubwa kama sauti ya muqawama.

Afif alikuwa mshauri wa muda mrefu wa vyombo vya habari wa marehemu Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyed Hassan Nasrallah, ambaye aliuawa katika shambulio la anga la Israel Septemba 27.

Alisimamia kituo cha televisheni cha al-Manar chenye uhusiano na Hizbullah kwa miaka kadhaa kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa vyombo vya habari katika harakati ya Hizbullah.

3490727

Kishikizo: hizbullah msemaji
captcha