IQNA

Jinai za Israel

Msemaji wa Hizbullah auawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Israel

19:06 - November 17, 2024
Habari ID: 3479766
IQNA-Mohammad Afif, msemahi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameuawa shahidi katika shambulio la utawala wa Kizayuni huko Ras al-Naba, Beirut mji mkuu wa Lebanon.

Afisa huyo mkuu wa habari wa Hizbullah ameuawa leo katika mashambulio ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya eneo la Ras al-Naba Beirut.

Wakati huo huo, Ali Hijazi, Katibu Mkuu wa Chama cha Kisochilositi cha Kiarabu cha Ba'ath, ameiambia Kanali ya Televisheni ya Al-Mayadeen kwamba: "shambulio dhidi ya ofisi yetu lilienda sambamba na vitisho vya mfululizo dhidi yetu tangu mwanzo wa vita. Hakukuwa na raia katika jengo hili. Tulifanya mikutano mingi katika jengo hili wakati wa vita na ilijulikana kwa kila mtu."

Huku akithibitisha kuuawa shahidi kwa afisa wa habari wa Hizbullah Mohammad Afif: "Kwa bahati mbaya alikuwakwenye jengo lililolengwa na aliuawa shahidi. Lengo la mashambulizi haya ni kunyamazisha vyombo vya habari na sauti ya kisiasa ya muqawama kwa sababu inawaudhi sana. Tunaunga mkono muqawama na bila shakka muqawama huu utashinda uwe siisi tupo au hatupo.

Harakati ya Hizbullah badoo haijathibitisha rasmi kuuawa shahidi afisa wakke huyo wa vyombo vya habari.

Katika mkutano wake wa mwisho na waandishi habari Jumatatu iliyopita, Afif alisema Hizbullah iko imara na inaendelea na mapambano ya kishujaa ya kulilinda taifa la Lebanon na kuwaunga mkono Wapalestina na kwamba ushahidi wa hilo ni jinsi wanajeshi vamizi wa utawala wa Kizayuni walivyokimbia kwa madhila na kutoka kwenye ardhi za kusini mwa Lebanon.
Alisema, wanamapambano wa Kiislamu wanaendelea kutoa vipigo vikali kwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni ambao wameshindwa kuiteka na kuikalia hata sehemu ndogo tu ya ardhi ya Lebanon licha ya majigambo makubwa wanayotoa mbele ya vyombo vya habari.
Aliongeza kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameamua kushadidisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya Lebanon hasa kusini mwa Beirut, ili kuficha fedheha ya kushindwa kwao vibaya kusini mwa Lebanon.

4248770

 

Habari zinazohusiana
captcha