Abdul Rahman Shadid alitoa wito huo jana Jumatatu baada ya vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuzifunga kwa wiki kadha sasa njia za kuingilia kambi ya Jenin inayowapa hifadhi Wapalestina wapatao 25,000, na kupambana na wanamuqawama walioko kwenye kambi hiyo.
Shadid amesema, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas ndiye anayebeba dhima ya "damu iliyomwagika" huko Jenin au kwenye maeneo mengine ya Ukingo wa Magharibi yakiwa ni matokeo ya kampeni ya mashambulio ya kijeshi iliyoanzishwa na Mamlaka yake ya Palestina.
Afisa huyo wa Hamas ameongeza kuwa, maafisa wa Mamlaka ya Ndani wanakataa kuitikia miito mbalimbali ya kitaifa na ushauri wa kukomeshwa mzingiro iliowekewa kambi ya Jenin na operesheni ya kijeshi inayotekelezwa na vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Ndani dhidi ya Muqawama katika Ukingo wa Magharibi,
Tangu mapema mwezi huu, askari wa usalama wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina wakisindikizwa na magari ya deraya wamekuwa wakishika doria katika kambi ya Jenin.
Askari hao wamewakamata Wapalestina kadhaa wenye mafungamano na makundi ya mapambano na Muqawama, hususan Brigedi ya Jenin na kupelekea kuzuka mapigano makali.
Makundi ya Muqawama yanasema, kinachofanywa hasa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina na vikosi vyake vya usalama ni kutekeleza matakwa ya utawala wa Tel Aviv huku kukiwa na ripoti kwamba kampeni hiyo ya kijeshi ya Jenin inaendeshwa chini ya uangalizi wa kijeshi wa Israel.
Wiki iliyopita, Hamas ililaani opereshenii ya kijeshi ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ikiita "uhalifu kamili," na kueleza kwamba silaha zinazotumiwa dhidi ya Wapalestina huko Jenin ingekuwa bora wangepatiwa wanamapambano wa Muqawama ili wakabiliane na wavamizi wa Kizayuni.
Katika taarifa yake, HAMAS imetoa wito wa kufanyika hamasa ya umma ya kuvunja mzingiro na kuwalinda wapiganaji wa Muqawama pamoja na kukabiliana na operesheni hiyo ya kijeshi, ambayo imesema, inatumikia jeshi vamizi la Israel.
4255803