IQNA

Kadhia ya Palestina

Makundi ya Palestina yafikia mapatano ya 'umoja wa kitaifa'

16:27 - July 23, 2024
Habari ID: 3479173
IQNA-Harakati ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, yenye makao yake huko Gaza imesema imetia saini makubaliano mjini Beijing na makundi mengine ya Palestina, ikiwa ni pamoja na Fat'h, kufanya kazi pamoja kwa ajili ya "umoja wa kitaifa."

Maafisa wa China wameyaelezea kama makubaliano yenye lengo la kudumisha utawala wa Palestina kuhusu Gaza.

Akizungumza Jumanne, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Mousa Abu Marzook amesema, “Leo tunatia saini mkataba wa umoja wa kitaifa na tunasema kwamba njia hii ni ya kukamilisha safari ya umoja wa kitaifa.

Ameyasema hayo baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na wajumbe kutoka makundi mengine ya Palestina, ambayo ni Fat'h, Harakati ya Jihad Islami, Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP) na Harakati ya Kidemokrasia kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (DFLP).

Wang, kwa upande wake, alisema wajumbe wa Palestina wamekubali kuunda "serikali ya muda ya maridhiano ya kitaifa" ili kutawala Gaza baada ya vita.

Tangazo la mapatano ya 'umoja wa kitaifa' wa Palestina linakuja zaidi ya miezi tisa baada ya Israel kuanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza kufuatia mashambulizi ya kushtukiza ya makundi ya wapiganaji wa Palestina katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

Hadi sasa utawala huo umewauwa takriban watu 39,006 wa Gaza, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na vijana. Wapalestina wengine 89,818 wamepata majeraha pia. China kwa muda mrefu imekuwa ikiunga mkono suala la Palestina.

3489228

Habari zinazohusiana
Kishikizo: palestina umoja hamas
captcha