IQNA

Kadhia ya Palestina

Hamas yakosoa misimamo ya Mamlaka ya Ndani Palestina

20:46 - February 21, 2023
Habari ID: 3476599
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema mapatano yaliyofikiwa karibuni baina ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala haramu wa Israel kwa mashinikizo ya Marekani ni usaliti kwa kambi ya muqawama ya Wapalestina.

Msemaji wa HAMAS, Abdulatif al-Qanou alisema hayo jana Jumatatu na kufafanua kuwa, hatua ya pande mbili hizo kuafikiana eti kusititisha harakati za kimapinduzi katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kutokana na mashininikizo ya Marekani inaenda kinyume na matakwa ya taifa la Palestina. 

Amesema kitendo cha Mamlaka ya Ndani ya Palestina cha kukubali hadaa na ahadi za njozi za Marekani mkabala wa eti Washington kuandaa na kuwasilisha katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa rasimu ya kulaani ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni, ni sawa na kulichoma jambi kwa nyuma taifa la Palestina, na kuwasaliti pia Wapalestina.

Kadhalika Msemaji wa HAMAS amepuuzilia mbali tangazo butu la Mamlaka ya Ndani la eti imesimamisha ushirikiano wake wa kiusalama na Israel na kueleza kuwa, mamlaka hiyo ingali ni tegemezi kwa utawala huo pandikizi, na imeendelea kutumbukia kwenye mtego wa hadaa na njozi za Marekani kwa gharama ya damu za Wapalestina.

Hivi karibuni pia, HAMAS ilitoa taarifa na kutangaza kuwa, kuendelea kamatakamata ya kiholela ya kisiasa dhidi ya viongozi na makada wa harakati hiyo, mateka na wanaharakati walioachiwa huru ni siasa zililizofeli na kugonga mwamba, na kwamba kitendo hicho ni sawa na kuuhudumia utawala wa Kizayuni. 

Duru za usalama za utawala za Kizayuni zimeeleza kuwa zinatiwa wasiwasi na kuongezeka operesheni za Wapalestina dhidi ya maeneo mbalimbali huko Israel  na kutahadharisha juu ya kupamba moto oparesheni hizo nje ya Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan katika miezi ijayo, sanjari na kushtadi harakati za makundi ya muqawama ya Palestina dhidi ya Israel. 

 

3482562

Kishikizo: hamas palestina
captcha