IQNA

Jinai za Israel

Vijana wawili Wapalestina wauawa shahidi katika makabiliano na askari wa Israel

18:02 - September 14, 2022
Habari ID: 3475782
TEHRAN (IQNA)- Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi vijana wawili wa Kipalestina kwa kuwapiga risasi kaskazini mwa eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu.

Jeshi la utawala haramu wa Israel limesema katika taarifa kuwa, Wapalestina hao wawili wameuawa mapema leo katika kituo cha upekuzi wa usalama karibu na kijiji cha Jalamah, kaskazini mwa jiji la Jenin, eneo la Ukingo wa Magharibi.

Taarifa hiyo imedai kuwa,  wanajeshi wa Brigedi ya Nahal waliwazingira wawili hao na kujaribu kuwakamata, lakini eti walilazimika kuwapiga risasi wakijibu ufyatuaji wa risasi uliofanywa na Wapalestina hao.

Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa, vijana hao wa Kipalestina waliouawa shahidi na Wazayuni ni Ahmed Abed na Abdul Rahman Abed, kutoka kijiji cha Kafr Dan karibu na Jenin.

Haya yanajiri baada ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) kutoa taarifa kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa 17 wa kutimuliwa Wazayuni kutoka Ukanda wa Gaza, ikisisitiza kuendelezwa mapambano ya Wapalestina hadi malengo yao ya mwisho yatakapofikiwa.

Gazeti la Kizayuni la Jerusalem Post limedai kuwa, mwanajeshi wa Israel ameuawa katika makabiliano hayo ya risasi baina ya wanajeshi wa Kizayuni na vijana hao wa Kipalestina mapema leo Jumatano kaskazini mwa Jenin. 

4085485

captcha