IQNA

Wapalestina washiriki maandamano makubwa kukumbuka kuanzishwa HAMAS + Picha

13:01 - December 11, 2021
Habari ID: 3474664
TEHRAN (IQNA)- Makumi ya maelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wameshiriki katika maadhimisho ya mwaka wa 34 wa kuasisiwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS).

Kwa mujibu wa duru za habari, makumi ya maelfu ya Wapalestina jana mchana walijitokeza kutoka kila kona ya Ukanda wa Ghaza na kushiriki katika maandamano makubwa ya kuadhimisha mwaka wa 34 wa kuasisiwa HAMAS.

Mushir al Masri ambaye ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema mbele ya wanachama wa harakati hiyo kwamba HAMAS itaendelea kutumia mbinu zote za muqawa katika kupambana na wavamizi wa Quds na amezilaumu zile nchi za Kiarabu zilizotangaza uhusiano wa kawaida na utawala katili wa Israel akisisitza kuwa, kufanya hivyo ni kuungana moja kwa moja na adui Mzayuni na ni usaliti kwa malengo matakatifu ya Palestina.

Kiongozi mwingine wa ngazi za juu wa HAMAS, Mahmoud al Zahar amesema katika maadhimisho hayo kuwa, tunayataka mataifa yote ya Kiarabu na Kiislamu kuunga mkono muqawama wa Palestina hadi ardhi zote zitakapokombolewa kutoka katika makucha katili ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Amesema, kutangaza uhusiano wa kawaida na Israel ni usaliti kwa ubinadamu na kwa mataifa huru duniani ambayo yanajitolea muhanga kupigania haki zao. 

Ameongeza kuwa, katika maadhimisho ya miaka 34 ya kuasisiwa kwake, sisi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS tunatangaza bayana kwamba kamwe hatutowaacha mkono mashujaa wetu walioko kwenye jela za Wazayuni.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS iliasisiwa na shahid Sheikh Ahmad Yasin tarehe 14 Novemba 1987.

 

4019892

captcha