IQNA

Qiraa

Idhaa ya Qur'ani Misri kurusha hewani Tarteel ya Sheikh Abdul Basit kwa mara ya kwanza

20:56 - December 27, 2024
Habari ID: 3479958
IQNA - Kwa mara ya kwanza, kuanzia Januari 2025, Idhaa ya Qur'ani ya Misri itarusha hewaniusomaji wa Tarteel wa Qur'ani kwa mtindo wa Warsh kutoka kwa simulizi la Nafi' na Qari mashuhuri wa Misri, Sheikh Abdul Basit Abdul Samad.
Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Cairo 24, Idhaa ya Qur'ani ya Misri ilitangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba matangazo hayo yataangazia usomaji wa Sheikh Abdul Basit katika Warsh kutoka kwa simulizi ya Nafi'.
Sheikh Abdul Basit Abdul Samad (1927-1988) alikuwa mmoja wa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani nchini Misri, anayejulikana kwa uwezo wake wa kipekee wa  kusoma Qur'ani kwa sauti ya kipekee na ya kupendeza.
Mara nyingi alijulikana kama "Sauti ya Makka." Mnamo 1984, alichaguliwa kama rais wa kwanza wa Muungano wa Wasomaji wa Qur'ani Misri. Katika maisha yake yote, alisafiri kimataifa, wakati wa Ramadhani na nyakati nyinginezo, ili kushiriki katika mikusanyiko ya Qur'ani na kuitikia mialiko.
3491228
captcha