IQNA

13:23 - May 22, 2022
Habari ID: 3475279
TEHRAN (IQNA)-Mvulana Mmisri mwenye umri wa miaka 9 ana kipaji cha kipekee cha kusoma Qur'ani Tukufu kiasi kwamba sasa amepewa lakabu ya 'Abdul Basit Mdogo".

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Misri, Omar Ali alianza kuvutiwa na usomaji Qur'ani Tukufu akiwa yungali mtoto mdogo.

Wazazi wake wanasema hakuna kilichoweza kumtuliza akiwa mtoto mchanga isipokuwa tu kusikiliza qiraa ya Qur'ani Tukufu.

Mama yake mzazi alikuwa akisoma Qur'ani muda mwingi wakati akiwa na ujauzito wa Ali.

 "Wakati akiwa na umri wa miaka saba tuligundua kuwa ana hami sana ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu," anasema baba yake Omar.

"Tulitaka sana kumpeleka shule binafsi ya msingi lakini alisisitiza kuenda katika shule ya Al Azhar na tulipomuuliza sababu alisema alitaka kuhifadhi Qur'ani Tukufu."

Kwa msaada wa mama yake, Omar aliweza kuhifadhi Juzuu 12 kwa muda wa mwaka moja na alipofika umri wa miaka 9 alikuwa amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Mvulana huyo mwenye kipaji anaishi katika Mkoa wa Giza nchini Misri na anasema lengo lake maishani ni kuwa msomi wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Al Azhar na pia daktari mpasuaji.

4058494

Kishikizo: Abdul basit ، qiraa ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: