IQNA

Uislamu na Ukristo

Papa Francis apokea maelezo kuhusu chuo kikuu cha Dini cha Iran

20:00 - March 14, 2023
Habari ID: 3476700
TEHRAN (IQNA) – Rais wa Chuo Kikuu cha Dini na Madhehebu za Kiislamu cha Iran amekutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani na kumfahamisha kuhusu shughuli cha chuo hicho.

Hujjatul Islam  Abolhassan Navvab  ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Papa Francis huko Vatican wiki hii.

Katika mkutano huo, mwanazuoni huyo Iran ametoa maelezo kuhusu  shughuli na sera za chuo hicho  akibainisha kuwa dhamira ya chuo hicho kikuu ni kuongeza ufahamu juu ya dini zote ili "kueneza amani na urafiki".

Kwa upande wake Papa Francis amebainisha kuwa uhusiano kati ya Uislamu na Ukristo umeimarika ikilinganishwa na siku za nyuma kutokana na juhudi za watu wote waliokanyaga njia hii.

Pia alionyesha kushangazwa na machapisho ya chuo kikuu hicho cha Iran, akibainisha kuwa hivi ndivyo manabii walivyofanya.

Papa Francis alisema Vatican inaunga mkono kuanzishwa kwa sehemu ya Ukristo katika chuo kikuu cha Iran.

Chuo Kikuu cha Dini na Madhehebu za Kiislamu, chuo kikuu cha kwanza kilichobobea katika uwanja wa dini na madhehebu nchini Iran, na kinalenga kueneza  maarifa ya dini na madhehebu na kujitahidi kwa mwingiliano na midahalo na wafuasi wa dini na madhehebu mbali mbali.

Chuo hicho chenye makao yake huko Qom kinalenga kufanya utafiti, na kutoa mafunzo kwa wataalamu ili kuleta mshikamano wa kibinadamu, kuimarisha amani, kupunguza mateso ya wanadamu, kueneza hali ya kiroho na maadili, na kutoa maelezo ya kitaaluma ya Uislamu kulingana na mafundisho ya kizazi cha Mtume Muhammad  SAW  yaani Ahlul-Bayt amani  ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao.

4127692

Kishikizo: papa francis navvab
captcha