IQNA

Qari wa Misri asoma Qur’ani Tukufu  kwenye  mkutano na Ayatullah Sayyid Ali Khamenei

14:35 - February 03, 2025
Habari ID: 3480152
IQNA – Washiriki, wajumbe wa jopo la majaji, na waandaaji wa Mashindano ya 41 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran walikutana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, mjini Tehran asubuhi ya  Jumapili.

 

Qari wa Misri Mohammad Hussein Muhammad asoma Qur’ani Katika mkutano 

Qari wa Misri Mohammad Hussein Muhammad, aliyeshika nafasi ya pili katika kipengele cha usomaji wa mashindano hayo, alisoma aya kutoka katika Qur’ani Tukufu wakati wa mkutano huo.

Alisoma Aya ya 38 hadi 48 za Surah Al-Ahzab, ambazo zinasema:

"Hakuna lawama kwa Nabii katika kufanya yale ambayo Mwenyezi Mungu amemfaradhishia. Huu ndio mwenendo wa Mwenyezi Mungu kwa wale waliopita kabla – na amri ya Mwenyezi Mungu ni amri iliyoamuliwa.

Wale waliokuwa wakifikisha ujumbe wa  Mwenyezi Mungu, wakimcha Yeye na wasimwogope yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mhasibu.

Muhammad si baba wa yeyote kati ya wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Manabii. Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.

Enyi waumini, mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi,

na mtukuzeni asubuhi na jioni.

Yeye ndiye anayewarehemu, na malaika wake wanawaombea ili awatoe kutoka gizani kuwapeleka kwenye nuru. Naye ni mwingi wa rehema kwa waumini.

Siku watakapokutana Naye, salamu yao itakuwa ‘Amani!’ – Malipo makubwa amewaandalia.

Ewe Nabii, hakika Tumekutuma kuwa shahidi, mtoaji wa bishara njema, na mwonyaji,

mwenye kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu kwa idhini Yake, na kama taa yenye kutoa mwangaza.

Wape waumini habari njema kuwa kwa Mwenyezi Mungu kuna fadhila kubwa kwao.

Usiwatii makafiri na wanafiki, wala usijali maudhi yao. Mweke Mwenyezi Mungu kuwa mlinzi wako; Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mlinzi."

 

 

 3491706

 

 

 

Kishikizo: qari
captcha