IQNA

Kituo cha kufundisha Qur'ani na masomo ya dini chazinduliwa nchini Mauritania

15:44 - February 06, 2025
Habari ID: 3480170
IQNA - Mnamo tarehe 5 Februari, kituo cha kufundisha Qur’ani, elimu ya dini, na lugha ya Kiarabu kilizinduliwa katika jiji la Nouakchott, mji mkuu wa nchi hiyo.

Kituo hicho, kilichopewa jina “Kituo cha Hajj Foudy Boubou Koreira”, kilianzishwa chini ya usimamizi wa Sidi Yahya Cheikhna Lemrabott, waziri wa masuala ya Kiislamu na elimu asili, kwa ufadhili kutoka kwa wahisani.

 Majengo haya yanajumuisha msikiti wenye uwezo wa waumini elfu moja, makaazi kwa wanafunzi na kiongozi wa maombi, majengo ya utawala, pamoja na miundombinu ya Awqaf ambayo mapato yake yatarudi kusaidia kituo hicho.

 Kwa mujibu wa Lemrabott, kituo hiki kikubwa cha Kiislamu kimeanzishwa kama sehemu ya mipango ya Wizara ya Masuala ya Kiislamu, inayotekeleza mpango wa Rais wa Mauritania Mohamed Ould Sheikh El Ghazouani unaoitwa "Ndoto Yangu kwa Taifa".

 Alisema kuwa wizara yake inatekeleza msururu wa mipango na miradi kusaidia misikiti kutekeleza jukumu lake la kukuza maadili, upendo, na udugu miongoni mwa jamii, kuimarisha mshikamano wa kitaifa, na kupambana na aina zote za tabia mbaya.

Mohammad Kurira, mkuu wa kituo kipya cha Kiislamu, alisema kuwa taasisi hii kubwa ya elimu itasaidia kueneza mafundisho ya Kiislamu na kupambana na mienendo hatari inayodhoofisha mshikamano wa kijamii na kuzuia maendeleo ya kiuchumi.

 Sherehe Yaadhimisha Mahafali ya Wahifadhi 130 wa Qur'ani nchini Mauritania

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika eneo la Magharibi  Afrika Kaskazini.

Inakadiriwa kuwa na idadi ya watu takriban milioni nne, na karibu wote ni Waislamu.

 Shughuli na programu za Qur'ani ni maarufu sana nchini humo. Mauritania ina historia ndefu ya hifdhi ya Qur’ani, na idadi ya wanawake wahifadhi wa Qur’ani na Hadithi ni kubwa sana, pengine kuliko nchi nyingine yoyote ya Kiislamu.

 

3491751

 

 

captcha