IQNA

Msikiti wa Jamkaran wapambwa kabla ya Idi ya Nisf Sha'ban 

15:03 - February 08, 2025
Habari ID: 3480176
IQNA –  Msikiti wa Jamkaran ulio katika mji wa Qom nchini Iran umepambwa kwa mataa ili kuutayarisha kwa ajili ya sherehe za siku ya katikati ya Sha’aban ambayo pia ni maarufu kama Nisf Sha'ban. 

Zaidi ya watu 20,000 kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Isfahan walihudhuria mkusanyiko huo siku ya Alhamisi. 
 
Familia za mashujaa kadhaa wa mkoa huo, wakiwemo Mashahidi Mohammad Reza Zahedi, Seyed Mohammad Hosseinzadeh Hejazi, na Abbas Nilforoushan, ziliheshimiwa katika hafla hiyo. 
 
Hafla hiyo pia ilijumuisha usomaji wa Dua ya Kumayl na Mehdi Mansouri pamoja na kaswida za kumsifu Ahl-ul-Bayt (AS). 
 
Katika siku zinazoelekea Sikukuu ya Mid-Shaaban, Msikiti wa Jamkaran huwa mwenyeji wa programu mbalimbali zinazoshirikisha watu kutoka tabaka mbalimbali za jamii. 
 
Sikukuu ya Nisf -Shaaban, inayoadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Zaman siku ya  kuzaliwa Imam Mahdi, ambaye ni Imamu wa kumi na mbili wa Waislamu wa madhehebu ya Shia ambaye pia anajulikana kama Imam Zaman (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake). huangukia tarehe 15 ya mwezi wa Shaaban katika kalenda ya Hijria ya Mwezi. 

 

3491775

 

captcha