IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Makka kwa Vikosi vya Jeshi

23:55 - February 11, 2025
Habari ID: 3480200
IQNA – Sherehe ya kufunga ya mashindano ya 10 ya kimataifa ya Quran kwa maafisa wa kijeshi ilifanyika katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia.

Luteni Jenerali Fayyad bin Hamed Al-Ruwaili, Mkuu wa Majeshi ya ya Saudia alitangaza washindi wa mashindano hayo katika hafla hiyo Jumapili usiku.

Katika hotuba yake, Musfer bin Hassan Al-Eisa, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Vikosi vya Jeshi la Saudi na msimamizi mkuu wa mashindano hayo, alirejelea juhudi za nchi yake za kukuza kuhifadhi Qur’ani na ufundishaji wa ufahamu wa ujumbe wa Qur’ani.

Alisema kuwa mashindano hayo yalitoa fursa kwa maafisa wa kijeshi wa nchi mbalimbali kushindana katika kuhifadhi na kusoma Qur’ani.

Pia alibainisha kuwa nakala 170,000 za Kitabu Kitakatifu zilisambazwa kati ya nchi zilizoshiriki katika mashindano hayo.

Washindi, wajumbe wa jopo la majaji na wale walioteuliwa kama wahudumu wa Qur’an Tukufu walienziwa mwishoni mwa sherehe.

Toleo la 10 la mashindano hayo lilihudhuriwa na wahifadhi wa Qur’ani 179 kutoka nchi 32.

Ilijumuisha kategoria sita: kuhifadhi Qur’ani kamili na kusoma kwa tajweed, kuhifadhi juzuu 20, 10, tano na tatu za Qur’ani na kusoma kwa tajweed, na pia kategoria ya usomaji mzuri zaidi kwa tajweed.

Washiriki mbali na mji wa Makka pia walizuri mji wa Madina, ambapo walitembelea maeneo ya kihistoria na kidini.

3491821

captcha