Harakati hiyo imesema katika taarifa yake: "Tunatoa wito kwa taifa letu, Umma wa Kiarabu na Kiislamu, na watu huru kote duniani, kufanya maandamano na kushiriki katika matukio ya kuonyesha mshikamano (na Wapalestina) katika miji na viwanja mbalimbali duniani, ili kupinga mipango ya kuwaondoa watu wetu wa Palestina kutoka katika ardhi yao."
Taarifa ya Hamas imeongeza kuwa: "Wacha Ijumaa, Jumamosi na Jumapili zijayo ziwe vuguvugu la kimataifa dhidi ya mipango ya kuwahamisha Wapalestina kwa kulazimishwa na mipango ya kuhamisha watu kwa mabavu inayopigiwa debe na utawala vamizi na watetezi wake."
Hamas imesisitiza kuwa shughuli hizi zinawakilisha himaya na uungaji mkono kwa haki za kudumu na halali za taifa la Palestina za kutetea ardhi yake, hasa haki yake ya uhuru, kujitawala, kujikombolewa na kujiamulia mambo yake.
Harakati hiyo imethamini misimamo ya kimataifa katika kuonyesha mshikamano na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Mnamo Februari 4, Rais wa Marekani, Donald Trump aliweka wazi nia ya nchi yake ya kuitwaa Gaza baada ya kuwafukuza Wapalestina kutoka eneo hilo na kuwahamishia katika nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Misri na Jordan.
Mpango huo wa Trump unaooana na mipango ya Wazayuni wa Israel ya kuwafukuza Wapalestina katika nchi yao, umwepingwa vikali na jamii ya kimataifa.
3491854