Haniyeh Barkhordari, kutoka mkoa wa kati wa Iran wa Yazd, ameshiriki katika hatua ya mwisho ya Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran katika kattegoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.
Akizungumza Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), amesema kwamba kuwa na vipaji haitoshi katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu kwa sababu mtu anahitaji pia kuwa na bidii, mwendelezo na ustahimilivu.
Wale wanaofaulu katika uwanja huu huvuna zawadi ya miezi au hata miaka ya juhudi, alisema.
Haniyeh amesema mama yake aligundua kipaji chake cha Qur'ani kwa mara ya kwanza na kumpeleka katika kituo cha Qur'ani akiwa na umri wa miaka 5.
Alianza kuhifadhi Quran kwa bidii akiwa na umri wa miaka tisa.
Alipoulizwa iwapo muda anaoutumia katika kuhifadhi Qur’ani umemzuia kufanya shughuli nyingine, alisema sivyo hata kidogo kwa sababu anatumia saa mbili hadi tatu tu kwa siku kwa ajili ya kujifunza Qur’ani.
Amesema kusoma Qur’ani kunampa utulivu na amani pamoja na hisia za furaha kubwa kwani maneno ya Kitabu hicho Kitukufu kimsingi ni mepesi.
Hinayeh alimnukuu mmoja wa walimu wake akisema kwamba mtu anapaswa kusoma Qur’ani ili kupata amani na kisha awazawadie wengine amani aliyopata.
Alibainisha kwamba yeye pia husoma Nahj al-Balagha na Sahifah Sajjadiyeh katika muda wake wa ziada.
Haniyeh alisema zaidi kwamba angependa kutumia muda zaidi katika kujifunza tafsiri ya Qur’ani na kukitafakari aya zake,
Duru ya mwisho ya Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran inaendelea katika mji wa kaskazini-magharibi wa Tabriz.
3490986