IQNA

Mashindano ya Qur'ani yafanyika Ghana kwa ushirikiano wa Iran

18:00 - April 30, 2022
Habari ID: 3475188
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yamefanyika nchini Ghana ambapo yamewashirikisha wanafunzi 60 wa vyuo vikuu.

Kwa mujibu wa  taarifa washiriki walikuwa ni wanafunzi wa kike na kiume ambao ni wanachama wa Jumuiya za Wanafunzi Waislamu katika Chuo Kikuu cha Ghana, Chuo Kikuu cha Kiislamu, Chuo Kikuu cha Lakeside na pia washiriki kutoka jamii za Nima na Mamobi.

Mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu yametayarishwa kwa pamoja na Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu cha Kanda mjini Accra na Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Accra.

Miongoni mwa wageni waliohudhuria mashindano hayo ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ghana, Bijane Gheraami, Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa Iran Mahmoud Khorshidi, Sheikh Mustapha Yaajalal ambaye ni msimamizi wa Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu cha Kanda ambaye pia ni imamu wa  Kituo cha Kiislamu cha Marzak Al Mihi.

Washindi watatu katikakategoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu wamepataza zawadi za fedha taslimu GH¢1500 (USD 199), GH¢ 1200 (USD 159) na GH¢1000 (USD 132) kwa taratibu pamoja na vitabu.

Balozi Gheraami amewapongeza washiriki kwa jitihada zao na amewasihi wajitahidi zaidi kuisoma Qur'ani Tukufu na kuifahamu kwa kina sambamba na kutekeleza mafundisho yake maishani.

4052705

captcha