Kwa mujibu wa taarifa hiyo, inatarajiwa kwamba mwezi mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani utaonekana jioni ya Jumamosi, Machi 1.
Hivyo basi, ofisi hiyo imetabiri kwamba Jumapili, Machi 2, 2025, itakuwa siku ya kwanza ya Mwezi wa Ramadhani
Ofisi ya Ayatullah Sistani katika mji mtakatifu wa Najaf pia imetabiri kwamba mwezi mwandamo wa mwezi wa Shawwal Hijri utaonekana jioni ya Jumapili, Machi 30.
Hii inamaanisha kwamba Ramadhani ya mwaka huu itakuwa na siku 29 na Idul-Fitr, ambayo inaashiria mwisho wa Ramadhani, itakuwa Jumatatu, Machi 31.
Ramadhani ni mwezi wa tisa na mtukufu zaidi katika kalenda ya Kiislamu, ambamo Waislamu wanakumbuka ufunuo wa Quran kwa Mtume Muhammad (SAW).
Wakati wa Ramadhani, Waislamu hufunga kutoka alfajiri hadi jioni, wakiepuka kula, kunywa, kuvuta sigara, na mahusiano ya ndoa.
Pia hutumia muda zaidi kwa ibada mbali mbali, kutoa sadaka, na matendo mema, wakitafuta kuimarisha imani yao na kutakasa roho zao.
Baadhi ya wasomi wa Kiislamu hutegemea mahesabu ya kinujumu au kianga ili kubaini mwanzo wa miezi ya mwandamo, wakati wengine wengi wanaamini kuwa kutazama mwezi kwa macho moja kwa moja au kutumia vifaa kama vile teleskopu ndiyo njia inayopaswa kutumika katika kubaini mwanzo na mwisho wa Mwezi wa Ramadhani.
3491926