IQNA

Jinai za Israel

Ayatullah Sistani wa Iraq asisitiza kusitishwa mauaji ya kimbari Gaza

11:50 - August 11, 2024
Habari ID: 3479262
IQNA - Kiongozi mkuu wa Kishia wa Iraq Ayatullah Sayyid Ali Sistani ametoa wito wa mshikamano na umoja kati ya mataifa ya Kiislamu kuchukua hatua kukomesha mauaji ya kimbari yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza na kuwasaidia watu wake.

Mwanazuoni huyo maarufu wa Kiislamu amelaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni ya kulenga shule iliyogeuzwa makazi katika mji wa Gaza na kusababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 100 na wengine wengi kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa ofisi ya Ayatullah Sistani, amesema jinai hiyo ya kutisha iliongeza tu katika orodha ya jinai zinazofuatana zilizotendwa na utawala wa Israel katika kipindi cha miezi kumi iliyopita.

Maneno hayatoshi kulaani uhalifu huo mbaya unaofanywa na wale ambao hawajui lolote kuhusu maadili ya Kiislamu na kanuni tukufu, alisema.

Kwa bahati mbaya, wanapata uungaji mkono usio na kikomo wa baadhi ya nchi kubwa zinazozuia utekelezwaji wa sheria za kimataifa kuhusu adhabu kwa wale wanaofanya uhalifu dhidi ya ubinadamu, alisikitika.

Vile vile alikashifu mauaji ya makamanda kadhaa wakuu wa muqawama ambaye amesema yamekiuka mamlaka ya baadhi ya nchi za kikanda na kusema kuwa hatua hizo zinaongeza hatari ya kuenea kwa migogoro katika eneo hilo.

Jeshi la utawala haramu wa Israel lilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya shule moja katikati mwa Mji wa Gaza wakati Wapalestina waliokimbia makazi yao walipokuwa wakiswali swala ya alfajiri siku ya Jumamosi na kuua takriban watu 100.

Bomu hilo lilipiga Shule ya Al-Taba’een wakati wa maombi katika kitongoji cha Daraj.

Utawala katili wa Israeli ulianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi Ukanda wa Gaza Oktoba mwaka jana na tokea wakati huo, kwa himaya ya Marekani, utawala huo umeua zaidi ya Wapalestina 40,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

3489447

Habari zinazohusiana
captcha