IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Aya za Kila Siku: Agizo la Mwenyezi Mungu la Kuwa Mwema kwa Wazazi

11:57 - March 27, 2023
Habari ID: 3476767
TEHRAN (IQNA) – Mwenyezi Mungu SWT amewataka wanadamu kuwa na huruma kwa wazazi wao, kwa mujibu wa aya ya 15 ya Surah Al-Ahqaf.

Daily Verses: God’s Order to Be Kind to Parents

Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapo fika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu. 

captcha