Ayatullah Sayed Yaseen al-Mousawi amesema Ayatullah Sistani ana nafasi kubwa katika kukwamisha njama za maadui na ndio maana wanalenga kukomesha nafasi hiyo yenye taathira.
Amesema utawala wa Kizayuni umekuwa ukipanga njama dhidi ya nchi za eneo kwa miaka mingi.
Utawala huo umetekeleza vitendo vingi vya kigaidi nchini Lebanon, yakiwemo mauaji ya Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrallah, alisema na kuongeza kuwa, utawala huo pia unajaribu kuiingiza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vita vya kila upande.
Al-Mousawi amesema Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni amekiri kuwa lengo la Israel si Palestina na Lebanon pekee bali inataka nchi zote za kieneo kuanzia Palestina hadi Iraq zidhibitiwe.
Ikizingatiwa kuwa Ayatullah Sistani ameuzuia utawala wa Israel kufikia malengo yake nchini Iraq, Tel Aviv imeweka jina lake katika orodha yake ya inaolenga kuwaua, msomi huyo amebaini.
Maadui hao wanajaribu kurudisha ugaidi wa Daesh (ISIL au ISIS) katika eneo ili kudhoofisha nchi za mhimili wa muqawama, alionya.
“Sisi ni watoto wa Imam Hussein (AS) na hatutaruhusu njama hizo. Maelfu ya vijana wa Iraq wamekuwa wakiniuliza siku hizi ni lini wakati utafika wa kupigana moja kwa moja na Wazayuni waliovamia Palestina,” ameongeza.
Mapema wiki hii, Kanali ya 14 ya Televisheni ya mrengo wa kulia ya Israel ilichapisha picha ya Ayatullah Sistani kama sehemu ya orodha ya walengwa wanaoweza kuuawa, na kuibua hasira za watu na maafisa wa Iraq, huku Waziri Mkuu Mohammed Shia Al-Sudani akisema hatua hiyo inaumiza hisia za Waislamu duniani kote.
3479567