IQNA

IAC yatangaza Mwezi wa Ramadhani utaanza Aprili 13

17:20 - April 04, 2021
Habari ID: 3473783
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kimataifa Kimataifa cha Nujumu (IAC) chenye makao yake mjini Abu Dhabi kimetangaza kuwa makadirio yanayoonyesha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 1442 Hijria Qamaria utaanza Aprili 13 2021.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya IAC mwezi mwandamo utaonekana Aprili 12 na hivyo siku itakayofuata itakuwa mwanzo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Nchi za Kiislamu ambazo kwa mujibu wa utabiri zitaweza kuuona mwezi mwandamo mnamo Aprili 12 bila tatizo ni pamoja na Algeria, Morocco, Mauritania, Iran, Indonesia, Malaysia, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Syria.

Naye Ibrahim al Jarwan, mwanachama wa Jumuiya ya Waarabu ya Nujumu na Sayansi za Anga za Mbali (AUASS) naye pia ametabiri kuwa aghalabu ya nchi zinatazamiwa kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mnamo Aprili 13. Amesema inatazamiwa kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani utakuwa na siku 30 na hivyo tarehe Mosi Shawwal inatazamiwa kusadifiana na Mei 13.

3474348

captcha