IQNA

Watu wa Austria watoa wito wa kususia Israel kutokana na mauaji ya kimbari Gaza  

20:47 - March 24, 2025
Habari ID: 3480427
IQNA – Jiji la Vienna, mji mkuu wa Austria, lilishuhudia maandamano makubwa yanayopinga kuendelea kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza. Waandamanaji walibeba mabango na vipeperushi vyenye maandiko, “Acha kuua watoto,” “Acha vita sasa,” na “Susia Israel."

Pia walikuwa wakitoa nara na kauli mbiu kama “La Kwa Mauaji ya Kimbari,” “Netanyahu Ni Muuaji,” na “Gaza Huru.” Washiriki wa maandamano walisisitiza kuunga mkono watu wa Palestina.

Mwandishi na mtetezi wa haki za binadamu nchini Austria Wilhelm Langthaler, aliyekuwa katika maandamano, alilaani utawala wa Israel kwa kuendeleza mauaji  dhidi ya watu wa Gaza. Alielezea vita vya Israeli dhidi ya Gaza kama janga kubwa na kusema kwamba watu wote wanashuhudia ukatili unaoendelea wa utawala wa Israeli wakati Magharibi inaendelea kuunga mkono Tel Aviv.

Alisisitiza kwamba watu wa Austria wanapinga genocide katika Gaza na wanataka kusitishwa mara moja vita katika eneo hilo la Palestina. Langthaler alieleza huzuni juu ya mgawanyiko mkubwa kati ya mitazamo ya serikali na vyombo vya habari nchini Austria na maoni ya umma kuhusu suala hili.

Hatutarajii msaada kutoka kwa serikali au vyombo vya habari, lakini tutajitahidi kuinua sauti ya Palestina, ubinadamu, haki, na demokrasia katika jamii yetu, na hakuna atakayetuzuia kufanya hivyo,” alihitimisha.

3492476

Habari zinazohusiana
captcha