IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Moscow Yamalizika

22:58 - November 21, 2022
Habari ID: 3476126
TEHRAN (IQNA) – –Mashindano ya 20 Kimataifa ya Kusoma Qur'ani ya Moscow yamekamilika katika hafla ya Jumapili usiku katika mji huo mkuu wa Urusi (Russia), ambapo walioshika nafasi za tatu za juu walitangazwa na kutunukiwa zawadi.

Msikiti Mkuu wa Moscow, ambao ulikuwa mahali pa mashindano hayo, pia uliandaa sherehe za kufunga Novemba 20.

Rais wa Baraza la Mufti wa Russia Sheikh Rawil Gaynutdin na mabalozi wa nchi za Kiislamu walikuwa miongoni mwa washiriki wakuu katika hafla hiyo.

Kulingana na tangazo la jopo la majaji, mwakilishi wa Uturuki Ahmed Kuzu aliibuka mshindi katika mashindano hayo

Mshindi wa pili alikuwa Abdul Rahman Faraj kutoka Misri na qari wa Iran Seyed Mostafa Hosseini aliibuka wa tatu.

Nafasi ya nne iilikwenda kwa qari aliyewakilisha Yemen.

Wasomaji wa Qur'ani kutoka nchi 21 zikiwemo Russia, Bahrain, Sudan, Umoja wa Falme za Kiarabu, Syria, Morocco, Tajikistan, Kazakhstan, Tanzania na Bangladesh walishiriki katika hafla ya kimataifa ya Qur'ani iliyoanza Ijumaa mjini Moscow.

Baraza la Mufti la Russia liliandaa hafla hiyo kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu..

Wajumbe wa jopo la majaji walikuwa wataalamu wa Qur'ani kutoka Yemen, Uturuki, Lebanon, Russia, na Saudi Arabia.

captcha