Akitoa shukrani zake, Khaby alisema, “Nataka tu kusema asante kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amenipa kila kitu na, muhimu zaidi, nguvu ya kuendelea na kuamini katika ndoto zangu.”
Alitafakari zaidi juu ya safari yake ya kibinafsi siku ya Jumamosi, na kuongeza, "Nimekabiliana na matatizo mengi maishani, na wakati kila kitu kilionekana kutowezekana, imani yangu ilinifanya nisimame."
Katika mahojiano ya awali na chombo cha habari cha Italia, nyota huyo wa mtandao wa kijamii mwenye umri wa miaka 22 alithibitisha imani yake, akisema, "Ndiyo, mimi ni Mwislamu, Mwislamu anayefungamana na mafundisho ya Kiislamu. sijui niseme nini kingine."
Mzaliwa wa Senegal, Khaby Lame alihamia Italia akiwa na umri wa mwaka mmoja tu. Akiwa na umri wa miaka 14, alisoma shule ya Qur'ani karibu na Dakar, Senegal, ambako alijitolea kusoma na kuhifadhi Qur’ani ambapo aliweza kuhifadhi Qur’ani kikamilifu.
Khaby alipata umaarufu duniani mwaka wa 2022 alipokuwa mtayarishaji wa maudhui anayefuatiliwa zaidi kwenye TikTok. Wakati huo, alikuwa na wafuasi milioni 143.2.
Maudhui anazosambaza Khaby, anayejulikana kwa klipu zake ucheshi zinazorahisisha mambo ambayo yanaonekana ni mafumu changamano wa maisha. Mtindo wake wa kipekee umempatia umaarufu mkubwa kati ya watazamaji mbalimbali duniani kote.
3491165