IQNA

Usomaji wa Ahmadi Wafa katika Tariq (Njia) ya al-Hussain (AS)

Msafara wa Qur'ani wa Noor ulifanya mikutano mingi ya qiraa ya Qur'ani Tukufu kwenye njia (Masir)ya kutembea ya Arbaeen 1444 kutoka Najaf hadi Karbala.

Waliokuwa katika msafara huo walisoma aya za Qur'ani Tukufu na klipu hii hapa chini ina qiraa ya aya za 5 hadi 13 za Sura Insan Hamidreza Ahmadi Wafa, msomaji wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mji wa Najaf Ashraf nchini Iraq.

 

 

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU


5. Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika na kafuri, 


6. Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi. 


7. Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,


8. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. 


9. Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. 


10. Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu.


11. Basi Mwenyna raha na furahaezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha. 


12. Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri. 


13 Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali. 

Kishikizo: arbaeen ، imam hussein