Kaulimbiu kuu ya mkutano huo wa siku mbili uliomalizika Alhamisi hii ni 'Udiplomasia wa Qur'ani, Kuelekea Katika Umoja wa Kiislamu'. Mkutano huo umehudhiriwa na wataalamu na watafiti wa masuala ya Qur'ani wa Senegal na Iran.
Profesa Chernoka Habib Habib ambaye ni mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Dakar amesema kuwa kufanyika mkutano huo ni miongoni mwa sababu za kuimarisha misingi ya umoja na mshikamano wa Kiislamu. Amesisitiza kuwa lengo la mkutano huo ni umoja na mshikamano baina ya Waislamu.
Kwa upande wake Sheikh Abdul Muniin Zein ambaye ni mjumbe wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema Uislamu unapinga kikamilifu vitendo vya ukatili na utumiaji mabavu na kwamba Qur'ani tukufu imejuzisha tu harakati na mapambano ya kujihami, kuilinda nafsi, mali na matukufu ya watu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkutano huo una anwani ya "Qur'ani Tukufu, Mwelekeo wa Kiroho na
Ulimwengu Usio na Ukatili", ulifunguliwa Jumatano mjini Dakar kwa himaya ya
Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Senegal