IQNA

Iran na Saudi Arabia zafikia mapatano kuhusu Hija

14:11 - December 19, 2018
Habari ID: 3471777
TEHRAN (IQNA) – Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia zimesaini Mapatano ya Maelewano (MOU) kuhusu kushiriki Wairani katika ibada ya Hija mwaka huu wa 1440 Hijria na 2019 Miladia.

Mapatano hayo yametiwa saini nchini Saudi Arabia Jumanne wiki hii baada ya mazungumzo baina ya Mkuu wa Shirika la Hija la Iran Alireza Rashidian na Waziri wa Hija wa Saudi Arabia Mohammad Saleh bin Taher Benten.

Katika mazungumzo hayo, Rashidian aliashiria baadhi ya matatizo ambayo Mahujaji Wairani walikumbana nayo katika Hija iliyopita na ametoa mapendekezo ya kuyasuluhisha.

Kwa upande wake Waziri wa Hija wa Saudi Arabia, amesema ameyasikiliza matatizo waliokuwa nayo Wiarani na ametoa hakikisho kuwa yatatatuliwa na hali ya Mahujaji itaboreka.

Kwa mujibu wa mapatano hayo, katika ibada ijayo ya Hija, Wairani 86,500 watapata idhini ya kutekeleza Ibada ya Hija. Mwaka uliopita Wairani 86,000 walifanikiwa kutekeleza ibada ya Hija na mwaka uliotanguliwa idadi hiyo ilikuwa 85,000. Kwa msingi huo idadi ya Wairani wanaopata idhini ya kutekeleza ibada ya Hija inazidi kuongezeka.

3773808

captcha