Mkuu wa Kituo cha Matibabu cha Hija cha Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran, Seyed Ali Marashi, alitoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Tehran siku ya Jumatano.
Amesema kuwa amesema 65 wana umri wa chini ya miaka 18, huku 8,500 wakiwa kati ya miaka 70 na 80. Idadi ya Wairani waliojisajili kuhuji walio chini ya miaka 40 ni ndogo.
Kuhusu wale ambao hali yao ya kiafya haikuthibitishwa kuwa inafaa kwa ibada hiyo, alisema watu 340 walionekana kuwa hawafai kiafya kushiriki katika ibada ya Hija mwaka huu.
Wale waliokata rufaa dhidi ya uamuzi huo walifanyiwa uchunguzi tena na tume ya kitaifa iliyokuwa na wataalamu, na hatimaye watu 73 walithibitishwa kuwa hawafai kiafya, alieleza.
Kuhusu maandalizi ya huduma za matibabu kwa mahujaji wa Iran katika Hija ya mwaka huu wa 1446 Hijria Qamaria saw ana 2025 Miladia, amesema maandalizi hayo yalianza zaidi ya miezi saba iliyopita.
Kwa Hija ya mwaka huu, daktari mmoja atatumwa Saudi Arabia kwa kila Mahujaji 550, amesema.
“Mwaka huu, misafara 643 iliundwa kwa ajili ya operesheni ya Hija, na kila daktari alikagua misafara mitatu, minne au mitano. Idadi ya madaktari waliowakagua mahujaji ni 154.”
Akiangazia muda uliobaki kabla ya kuanza kwa Hija, Marashi amewashauri wanaoelekea Hija kuanza kufanya mazoezi ya kutembea mara kwa mara ili kuimarisha afya zao, na pia kuhakikisha wanabeba dawa zao za kutosha ambazo zitawatosha hadi baada ya kukamilika kwa ibada yao Saudi Arabia.
Hija ni safari ya hija katika mji mtakatifu wa Makka ambayo kila Mwislamu mwenye afya njema na uwezo wa kifedha anatakiwa kuitekeleza angalau mara moja maishani.
Hija ya kila mwaka inachukuliwa kuwa ni moja ya nguzo za Uislamu na ndiyo ibada kubwa zaidi ya pamoja duniani. Pia ni ishara ya umoja wa Waislamu na utiifu wao kwa Mwenyezi Mungu (Allah).