Operesheni iliyofanyika kati ya tarehe 3 hadi 9 Aprili iliwakamata watu 18,669 nchini kote, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.
Mamlaka ziliarifu kwamba waliokamatwa walikiuka sheria za makazi, kazi, na mipaka. Hatua hizi zinachukuliwa wakati Saudi Arabia inajiandaa kupokea mamilioni ya waumini kwa ajili ya Hija, ibada ya kila mwaka ya Kiislamu ya kwenda Makka, ambayo mwaka huu inatarajiwa kuanza tarehe 4 Juni, 2025, inayolingana na tarehe 8 Dhu al-Hijjah kwenye kalenda ya Kiislamu.
Wizara ilithibitisha kuwa watu 11,813 walikamatwa kwa kukiuka sheria za makazi, 4,366 kwa ukiukaji wa kanuni za usalama wa mipaka, na 2,490 kwa ukiukaji wa sheria za kazi.
Miongoni mwa waliokamatwa, 1,497 walinaswa wakijaribu kuingia Saudi Arabia kinyume cha sheria. Kati ya hao, asilimia 69 walikuwa raia wa Ethiopia, asilimia 27 wa Yemen, na asilimia nne walikuwa kutoka nchi zingine. Aidha, watu 59 walizuiliwa wakijaribu kuondoka Saudi Arabia kwa njia isiyo halali.
Wizara ya Mambo ya Ndani ilitoa onyo la umma kwamba yeyote atakayesaidia wakazi haramu anaweza kukabiliwa na adhabu kali.
Adhabu hizo zinajumuisha hadi miaka 15 gerezani, faini ya hadi Riyal milioni 1 za Saudi (karibu USD 266,000), na kunyang'anywa gari au mali yoyote iliyotumika katika kosa hilo.
3492674