IQNA

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Utawala wa Kizayuni umejiandalia hatima chungu na yenye maumivu

9:33 - June 13, 2025
Habari ID: 3480828
IQNA-Katika taarifa ya kulaani shambulio lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ardhi tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema leo alfajiri, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ametoa ujumbe mzito kwa taifa la Iran, akisisitiza kuwa adhabu kali inamsubiri mhalifu huyo wa kimataifa.

Kwa mujibu wa tovuti ya khamenei.ir, Ayatullah Khamenei amesema kuwa Mashambulizi hayo ya alfajiri yaliyolenga maeneo ya raia, yamedhihirisha kwa mara nyingine asili ya kikatili ya utawala wa Kizayuni.

Hii hapa matini ya ujumbe huo

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

“Enyi watu wa Iran,
"Mapema alfajiri ya leo, utawala wa Kizayuni umeonesha uso wake wa kweli kwa kutekeleza jinai dhidi ya nchi yetu pendwa. Kwa mikono yake iliyochafuka kwa damu, umevamia maeneo ya raia na kufichua zaidi tabia yake ya kikatili.

Utawala huu lazima usubiri adhabu kali. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, mkono wenye nguvu wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu hautamuacha (Mzayuni)."

Baadhi ya makamanda wetu mashujaa na wanasayansi wameuawa shahidi wakilitumikia taifa. Makaimu na wafanyakazi wenzao waliobaki wataendelea kutekeleza majukumu yao bila kusita, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Kwa jinai hii, utawala wa Kizayuni umejiandalia hatima ya uchungu na mateso. Bila shaka watakumbwa nayo.

Sayyid Sayyid Ali Khamenei

Juni 13 2025

4288154

captcha