Leo ni siku ya kwanza ya mwezi wa Hijri wa Muharram nchini Iraq.
Mustafa Murtadha Ziyaeddin, mfawidhi wa kaburi la Aba Al- Fadhl Al-Abbas (AS) huko Karbala, alibadilisha bendera nyekundu katika kaburi hilo na ile nyeusi kulingana na mila ya muda mrefu.
Bendera nyeusi inaashiria maombolezo ya Waislamu wa Shia kwa ajili ya kuuawa shahidi Imam wa tatu (AS).
Muharram ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwandamo ya Hijri.
Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengineo katika sehemu mbali mbali za dunia huomboleza kila mwaka katika mwezi wa Muharram katika kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba zake.
Bendera ya Haram ya Imam Ridha (AS) nchini Iran nayo pia Ilibadilishwa katikati ya Maandalizi ya Muharram
Imamu wa tatu wa Shia ambaye ni Imamu Hussein (AS) na kikundi kidogo cha wafuasi wake na wanafamilia wake waliuawa kishahidi na kidhalimu katika zama utawala wa Yazid Bin Muawiya, katika vita vya Karbala katika siku ya kumi ya Muharram (ijulikanayo kama Ashura) mwaka wa 61 Hijria sawa 680 Miladia.
3489049