IQNA

Kuhifadhi Qur'ani Tukufu

Msichana wa Kipalestina ahifadhi Qur'ani ndani ya mwezi mmoja

14:43 - August 17, 2022
Habari ID: 3475635
TEHRAN (IQNA) – Ilimchukua msichana wa Kipalestina mwezi mmoja tu kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu katika hatua amabyo imetajwa kuwa ni ya aina yake.

Msichana huyo kwa jina Jani Adham Naeem Ashur, ana umri wa miaka 13, na anatoka Ukanda wa Gaza.

Hafla ilifanyika hivi karibuni ambapo alienziwa na maafisa wa Qur'ani wa eneo hilo kwa mafanikio yake makubwa.

Hafla hiyo iliandaliwa na taasisi ya kutoa misaada ya Qur'ani ya Iqra, ambayo rais wake alibainisha matarjio  yake kwamba binti huyu aliyehifadhi Qur'ani atautumikia Uislamu na Qur'ani Tukufu.

Habari za kufanikiwa kwa Jani zimeenea kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu hazijawahi kutokea. Hakuna mtu mwingine anayejulikana kuwa aliweza kuhifadhi Qur'ani yote ndani ya mwezi mmoja tu.

Qur'ani Tukufu ndio Maandiko pekee ya kidini ambayo yanaweza kuhifadhiwa kikamilifu na wafuasi wake.

Watu wasiohesabika katika kila umma wa Kiislamu wamehifadhi Qur'an tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa.

Quran ina Juzuu (sehemu) 30, Sura (sura) 114 na aya 6,236, kwa hivyo kuhifadhi Kitabu kitakatifu kizima si kazi rahisi.

3480125

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha