IQNA

Waislamu milioni moja kutekeleza Ibada ya Hija mwaka huu

16:58 - April 09, 2022
Habari ID: 3475104
TEHRAN (IQNA)- Mamlaka ya Saudia ilitangaza Jumamosi kwamba nchi hiyo itawaruhusu Waislamu milioni moja kushiriki katika ibada inayokuja ya Hija.

Saudi Arabia ilisema Jumamosi itawaruhusu Waislamu milioni moja kutoka ndani na nje ya nchi kushiriki katika Hija mwaka huu, hii ikiwa ni idadi kubwa zaidi baada ya vizuizi vya janga la corona kulazimisha kupunguzwa idadi ya mahujaji katika kipindi cha miaka miwili mfululizo.

Wizara ya Hija imesema katika taarifa yake kuwa "imeidhinisha mahujaji milioni moja, wa kigeni na wa ndani, kutekeleza ibada ya hija mwaka huu."

Moja ya nguzo tano za Uislamu, Hija inapaswa kutekelezwa na Waislamu wote wenye uwezo angalau mara moja maishani. Hija kwa kawaida huwa  moja ya mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini ulimwenguni, ambapo mwaka 2019 takriban Waislamu milioni 2.5 walishiriki katika ibada hiyo.

Lakini baada ya kuanza kwa janga la coronavirus mnamo 2020, viongozi wa Saudi waliruhusu mahujaji 1,000 tu kushiriki.

Mwaka uliofuata, waliruhusu tu wakaazi wa Saudia kushiriki katika ibada ya Hija ambapo washiriki 60,000 waliochanjwa kikamilifu waliochaguliwa kupitia bahati nasibu

Vizuizi hivyo hivyo vya Hija vilivyowekwa na Saudia vimekosolewa sana  Waislamu walio nje ya nchi ambao walizuiliwa kushiriki ibada ya Hija mwaka jana. Tangazo la Jumamosi lilisema kuwa hajj ya mwaka huu itakuwa tu kwa mahujaji walio na chanjo na ambao wana  umri wa chini ya miaka 65.

Wale wanaotoka nje ya Saudi Arabia watahitajika kuwasilisha matokeo hasi ya Covid-19 PCR kutokana na kipimo kilichochukuliwa ndani ya saa 72 kabla ya kusafiri.

Serikali inataka kuhakikisha usalama wa mahujaji "huku ikihakikisha kwamba idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani kote wanaweza kutekeleza hajj", taarifa ya Jumamosi ilisema.

3478417

Kishikizo: saudi arabia hija
captcha